Chituz
MOSES OPUDO.
Leo NI siku ya furaha,
Ni siku iliyotengwa ya Buraha,
Musa amemaliza mwendo BILA jeraha.
Mola akulinde Pasta Musa,
Azidi kukubariki,
Ulikuwa Mwalimu na pia rafiki,
Kazi zako ulihakiki,
Aliitwa Pasta MOSES OPUDO.
Sala zako daima tutazikumbuka,
Uliomba Kwa dhati na uhakika,
Neno la Bwana ulifanya wengi wakalishika.
Mola akulinde Pasta Musa,
Azidi kukubariki,
Ulikuwa Mwalimu na pia rafiki,
Kazi zako ulihakiki,
Aliitwa Pasta MOSES OPUDO.
Hatutawahi kusahau zako suti.
Ulikuwa nadhifu pamoja na zako njuti,
Kweli fundi alivuta futi!
Ulikuwa na uko Smati!
Mola akulinde Pasta Musa,
Azidi kukubariki,
Ulikuwa Mwalimu na pia rafiki,
Kazi zako ulihakiki,
Aliitwa Pasta MOSES OPUDO.
Ulifunza Hadi ukawa Mwalimu Mkuu,
Hizi NI baraka kutoka juu.
Mama Opudo Mzee umekaa juu.
Mola akulinde Pasta Musa,
Azidi kukubariki,
Ulikuwa Mwalimu na pia rafiki,
Kazi zako ulihakiki,
Aliitwa Pasta MOSES OPUDO.
Upendo wako Kwa wote Pasta Musa,
Ulijulikana Sana wala hukuwa na visa,
Si huku Tu Hadi Kwa kanisa.
Mola akulinde Pasta Musa,
Azidi kukubariki,
Ulikuwa Mwalimu na pia rafiki,
Kazi zako ulihakiki,
Aliitwa Pasta MOSES OPUDO.
Baraka za Rabuka zikufikie,
Neema za Mola zikuonekanie,
Musa umejaliwa,
Musa baraka umepatiwa.
Tutazidi kukumbuka na mema.
Mola akulinde Pasta Musa,
Azidi kukubariki,
Ulikuwa Mwalimu na pia rafiki,
Kazi zako ulihakiki,
Aliitwa Pasta MOSES OPUDO.