Frobits
🎵 A song made on Frobits

Njooni Kwangu

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

Njooni kwangu, njooni kwangu
Msumbukao na kulemewa
Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa
Na mizigo mizigo ya dhambi, niwapumzishe asema Bwana
Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi
Nanyi mtapata raha, raha mioyoni mwenu
Unangoja nini wewe, unangoja nini
Unangoja nini ndugu yangu wewe
Unataka nini ndugu yangu
Mbeba mizigo anakuita
Tua mizigo yako msalabani
Acha mambo yote yaliyo machukizo
Mbele zake Mungu mfuate Yesu
Sauti yake Yesu tena ni ya upole
Inakubembeleza mfuate Yesu
Enyi ndugu sikilizeni nyote
Wito wake Yesu mwokozi
Anasema tua mizigo yako
Usiache hata kidogo
Hata ile dhambi uipendayo
Uiache Yesu anasema
Uje kwa Yesu apumzishwe
Amekungoja wewe siku nyingi
Unangoja nini mama
Unangoja nini ndugu yangu wewe
Unataka nini ndugu yangu
Mbeba mizigo anakuita
Tua mizigo yako msalabani
Acha mambo yote yaliyo machukizo
Mbele zake Mungu mfuate Yesu
Sauti yake Yesu tena ni ya upole
Inakubembeleza mfuate Yesu
Njooni kwangu, njooni kwangu
Mtapata raha mioyoni mwenu

More songs by Mwl. Listen to songs created by others
FROBITS