Ebenezer, umenifikisha hapa.
Haleluya, wastahili sifa.
Kutoka chini kabisa Bwana umeninyanyua
Ukanipa nafasi leo ninasimama
Ukatumia watu kugusa maisha yangu leo
Mimi si yule wa jana, jina lako naliinua
Haleluya, Bwana asifiwe!
Umenifanya kiumbe kipya, Ebenezer!
Hata hapa ni kwa mkono wako, Yehova!
Nalilinda jina lako, wastahili sifa zote
Unastahili, asante Yesu!
Linda familia yangu kwa mkono wako wa amani
Nifundishe unyenyekevu, kuwa mtumishi sio bwana
Palipo na chuki niletee upendo wako
Nibariki kwa utajiri ili nitende kazi yako
Amina, niongoze Baba!
Umenifanya kiumbe kipya, Ebenezer!
Hata hapa ni kwa mkono wako, Yehova!
Nalilinda jina lako, wastahili sifa zote
Unastahili, asante Yesu!
Hata hapa ni wewe Yehova.
Mtumishi wako niko tayari.
Amina, amina.