Chriss Msaki Nasifu kuwa Mtafuteni Bwana maadamu yeye anapatikana yeye yu karibu Bwana Anapatikana yeye yeye yu karibu
Kiitikio
Mtafuteni Bwana maadamu yeye anapatikana yeye yu karibu Bwana Anapatikana yeye yeye yu karibu x2
Ubeti
Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisaLakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Kiitikio
Mtafuteni Bwana maadamu yeye anapatikana yeye yu karibu Bwana Anapatikana yeye yeye yu karibu
Mtafuteni Bwana maadamu yeye anapatikana yeye yu karibu Bwana Anapatikana yeye yeye yu karibux2
Ubeti
Kutegemea ni kuweka tumaini kwa Mungu, mtu, kitu au vitu. Unaweka tumaini ukijua kuwa hao wana uwezo zaidi yako na wanaweza kukusaidia hasa pale unapokuwa kwenye mambo magumu au mazito.BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Ee BWANA, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha BWANA, kisima cha maji yaliyo Kumtegemea mwanadamu huleta laana au kulaaniwa na BWANA.
Unafanyika laana kwa sababu ya kutoa nafasi ya Mungu ndani yako na kumpa wanadaamu mwenzako ambaye naye ameumbwa na Mungu pia. Mungu anataka ategemewe yeye peke yake pasina kuchanganya na mwingine yeyote yule
Kiitikio
Mtafuteni Bwana maadamu yeye anapatikana yeye yu karibu Bwana Anapatikana yeye yeye yu karibu
Mtafuteni Bwana maadamu yeye anapatikana yeye yu karibu Bwana Anapatikana yeye yeye yu karibux2