Eeh Mungu, uongoze hatua zetu
Grade Eight Winners, ndoto zetu ziko mikononi mwako
Halleluya!
Kwenye madawati tunasoma kwa bidii
Tukiwa na imani, hatuna hofu kamwe
Grade Eight Winners tunainuka sasa
Mungu ametupaka mafuta ya ushindi
Tunaona mwangaza mbele yetu
Kesho yetu ni kuu na ya baraka
Sisi ni viongozi wa kesho (Amina!)
Tutaongoza kwa upendo na haki
Mungu ametuchagua, Grade Eight Winners
Kuangaza gizani, sifa zivume!
Halleluya, tutafika mbali!
Milima itasogea kwa jina la Yesu
Kila ndoto yetu itatimia kweli
Tutatetea wanyonge, tutaleta amani
Tukiwa na nguvu za Roho Mtakatifu
Hakuna wa kuzuia ushindi wetu leo
Sisi ni viongozi wa kesho (Amina!)
Tutaongoza kwa upendo na haki
Mungu ametuchagua, Grade Eight Winners
Kuangaza gizani, sifa zivume!
Halleluya, tutafika mbali!
Tunaongozwa na viongozi wetu wa daraja ambao wameonyesha uongozi WA juu,wakiongozwa na Issa John,Equinox Judy na mwalimu wa daraja Bi.Shamim About.
Kwa michezo tumetia fora,kama Shylex Anita na Brighton Owen kwa mchezo wa vikapu,kwa kandanda Avidon,Barack,Anyanga na Nancy.Sitasahau Jack muzethi wa handiboli, Kennedy Wigina wa volipoli hauwezi kuachwa nyuma
Matokeo kwenye mtihani ni wazi ndoto yetu itatimia.tujikaze kisabuni kesho yetu itangaa.walimu wetu tunawapongeza kwa kazi yenu nzuri tumeahidi kufanya bidii hatutawaibisha hata kidogo
Ndoto zetu ni hai,tuzipalilie
Grade Eight Winners, viongozi wa kesho!
Amina, Halleluya!