Umewahi kutafakari?
Umewahi kutafakari juu ya Upendo wa Mungu kwako
Alivyotupenda wanadamu katufanya sisi ni dhamani
Kamtoa mwanawe Yesu Kristo, katufia msalabani, ili kutukomboa wanadamu kutoka kwenye utumwa wa dhambi.
Umewahi kutafakari na ule upendo wa Yesu
Kakubali mateso hata mauti ya msalaba
Ili kutumboa wanadamu kutoka kwenye utumwa wa dhambi.
Sasa tutulie tusikie Neno la Mungu linasema nini nasi juu ya maisha yetu ya wokovu
Neema ya wokovu inapatikana sasa
Njoo kwa Yesu ndugu Neema yake bado ipo
Njoo kwa Yesu ndugu Neema yake ingali ipo
Ukimkiri kwa Kinywa ya kwamba yeye Bwana na kuamini moyoni utaokolewa
Ukimkiri kwa Kinywa ya kwamba yeye Bwana na kuamini moyoni utaokolewa
Bwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli
Mtakuwa na amani, upendo na furaha.
Bwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli
Mtakuwa na amani, upendo na furaha.
Acha kusumbukia dunia ndugu
Acha kusumbukia dunia ndugu
Acha kusumbukia dunia ndugu utapotea, njoo kwake Yesu
Ili tukamlaki mawingunj sikubile ajapo
Tutafurahi pamoja na Bwana Yesu
Tukizunguka kiti cha enzi yake
Atatufuta machozi yote Bwana
Atatukaribisha enzini pake
Njooni tufurahie pamoja
Njooni tufurahie pamoja
Njooni tufurahie pamoja
Kwa furaha na Bwana wetu Yesu
Furaha ya milele Amina!!