Halleluya, Amina!
Yesu Kristo, Mwokozi wetu.
Mwokozi wangu ulikwenda mbinguni,
Kuketi pamoja naye Baba.
Utakusanya sisi sote huko,
Mbinguni kwako utufikishe!
Makao mema watuandalia,
Unatungoja nyumbani kwa Baba!
Makao mema watuandalia,
Unatungoja nyumbani kwa Baba!
Mwombezi wetu wewe, Yesu Kristo,
Hutuombea kwa Mungu Baba.
Unatuchunga sisi, kundi lako,
Watusaidia jaribuni.
Na siku zote unatuombea,
Watushindia vita kali huku.
Makao mema watuandalia,
Unatungoja nyumbani kwa Baba!
Makao mema watuandalia,
Unatungoja nyumbani kwa Baba!
Ulivyokwenda ndivyo utarudi,5
Niombe, nikakeshe kwa imani.
Amina, Halleluya!