Nilitoka mbali, gizani nikipotea
Dhambi zangu nyingi, moyo ukiwa mzito
Lakini sauti yake ikanita kwa upole
“Mtoto wangu njoo, msalabani kuna uzima”
Sikuwa na cha kutoa, mikono yangu mitupu
Matendo yangu yote, hayakutosha kuniosha
Ila damu yake ikashuka, ikaniweka huru
Leo nasimama kwa Neema, si kwa haki yangu
Tunaokolewa kwa neema, neema ya Kristo YESU
Si kwa matendo yetu, bali kwa upendo Wake
Ametulipa gharama yote, msalabani Kalvaria
Halleluya, tumeokolewa, neema imetutosha!

Dunia iniseme nini, nilishindwa mara ngapi
Sheria ikanihukumu, ikanifunga pingu
Lakini YESU akaja, akazivunja zote
Akanipa jina jipya, akaniita mwanaye
Tunaokolewa kwa neema, neema ya Kristo YESU
Si kwa matendo yetu, bali kwa upendo Wake
Ametulipa gharama yote, msalabani Kalvaria
Halleluya, tumeokolewa, neema imetutosha!
Tunaokolewa kwa neema, neema ya Kristo YESU
Si kwa matendo yetu, bali kwa upendo Wake
Ametulipa gharama yote, msalabani Kalvaria
Halleluya, tumeokolewa, neema imetutosha!
Neema, neema, inanitosha mimi
Kila siku hunivisha, haki isiyo yangu
Neema, neema, ya Bwana wa Mabwana
Hakuna hukumu tena, kwa walio ndani ya Kristo
Tunaokolewa kwa neema, neema ya Kristo YESU
Si kwa matendo yetu, bali kwa upendo Wake
Ametulipa gharama yote, msalabani Kalvaria
Halleluya, tumeokolewa, neema imetutosha!
Tunaokolewa kwa neema, neema ya Kristo YESU
Si kwa matendo yetu, bali kwa upendo Wake
Ametulipa gharama yote, msalabani Kalvaria
Halleluya, tumeokolewa, neema imetutosha!
Simply jesus, jesus plus nothing.
The grace walk...