Frobits
🎵 A song made on Frobits

Tathmini ya Hijja 2026

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

Bismillah naanza, kwa Mola wetu muweza, (ah!)
Nataka kuendeleza, haya niliyokusudia.
Ya Ilahi ya Manani, mtukufu Rahmani,
Kwako ndio maskani, yafaa kukusudia.
Twaanza na shukrani, zilizojenga moyoni,
Hawa viongozi wetu, washika mikono yetu.
Tukitua Saudia, milango twafunguliwa, (ndugu!)
Ibada yetu ya Hijja, ni ibada ya mwangaza.
Subira kitu cha mbele, wazee na wanavyele, (ay!)
Uidumishe milele, mkobani kuitia.
Mola tupe afya njema, na elimu isokoma,
Twaomba kwako Rabana, takabali zetu dua!
Hija ni nguzo ya tano, nguzo hii ngumu mno,
Hutiwa kwenye mabano, subira kujaribiwa.
Shekhe wetu wa bobea, Suwedi hebu sogea, (ah!)
Na daktari wetu Saleh, huduma zake kutoa.
Mahujaji waungwana, nyumbani mwarudi tena,
Ikhlasi ndio nguo, ya kuvisha muilio.
Subira kitu cha mbele, wazee na wanavyele, (ay!)
Uidumishe milele, mkobani kuitia.
Mola tupe afya njema, na elimu isokoma,
Twaomba kwako Rabana, takabali zetu dua!
Hapa mie nikomele, Rabbi akinijalia,
Itikieni amina, Mola kuzikubalia. (Amina!)

More songs by MSA Listen to songs created by others
FROBITS