Eeh baba, ni mwarabu kwenye hii tena naimba
Tuimbe wote wanangu
Mnaniinua wakati ninavyoanguka chini
Mnanipa nguvu za kwenda mbele bila wasiwasi
Nyinyi ni familia, marafiki, ndugu zangu wa kweli
Kwa furaha na huzuni, daima mpo pembeni
Mnanipa juhudi za kufanya kila kitu
Mnanionyesha upendo bila kujali udhaifu
Watu wangu wa nguvu, nyinyi ni hazina yangu
Ninawapenda sana, mimi bila nyinyi si kitu
Watu wangu wa nguvu, faraja moyoni mwangu
Asante kwa kila kitu, nyinyi ni baraka yangu
Tukutane mahali popote, mnanifanya najisikia nyumbani
Maneno yenu yananiinua juu kama ndege angani
Mnanishika mkono wakati dunia inageuka giza
Nyinyi ni nuru yangu, mwangaza wa maisha
Kila siku ninashukuru kwa kila jambo
Mnafanya safari hii kuwa tamu zaidi
Watu wangu wa nguvu, nyinyi ni hazina yangu
Ninawapenda sana, mimi bila nyinyi si kitu
Watu wangu wa nguvu, faraja moyoni mwangu
Asante kwa kila kitu, nyinyi ni baraka yangu
Twende pamoja, kwa upendo
Upendo huleta furaha na nuru mpya
Nyinyi ni watu wangu wa maana, familia yangu halisi
Kwa ajili yenu naimba na hii tena eeh!, meneja ben dani lavalava edah na Noah msijali familia denis fundi ande sokolo Angel NA eliza wa Mjomba wote sema eeh! , suma rush wapi seinangai damasi wazee wa kazi hii ni yenu wanangu Gibson cheusi Alex Tuimbe wote
Watu wangu wa nguvu, safi sana
Asante kwa kila kitu,
Nyinyi ni kila kitu kwangu, eeh!
Ni mwarabu kwenye hii tenaa