Frobits
🎵 A song made on Frobits

Umoja Ni Nguvu

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

*UMOJA NI NGUVU, TUKIWA PAMOJA TWASHINDA.*
Umoja ni nguvu,
Tukiwa pamoja twashinda (aaah!!)
Pamoja tujenge kanisa la Bwana (aaah!!)
Sisi sote twategemeana Katika maisha..
Hakuna aliye bora kuliko mwingine, twategemeana
Kila mmoja weetuuu
Amuhitaji mwenzake
Seremala kumtia moyo mfua dhahabu
Alainishaye kwa nyundooo
Amuhimize apigaye fuawe..
Aisifu kazi ya kuunga ya kuwa ni njema
Kushirikiana kutiana moyo
Mwili wa kristo twaujenga sote!!
Umoja ni nguvu,
Tukiwa pamoja twashinda (aaah!!)
Pamoja tujenge kanisa la Bwana (aaah!!)
Umoja ni nguvu,
Tukiwa pamoja twashinda (aaah!!)
Pamoja tujenge kanisa la Bwana (aaah!!)
Bwana wetu Yesuuu
Katuombea umojaaa
"Nami Utukufu ulionipa
Nimewapa wao
Ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja"
Hayo ni maneno ya Yesu
"Mimi ndani yao
Nawe ndani yangu
Ili wawe wamekamilika katika umoja
Ili ulimwengu ujue ndiwe uliyenituma
Ukawapenda wao
Kama ulivyonipenda mimi" (iìiiih)
Umoja ni nguvu,
Tukiwa pamoja twashinda (aaah!!)
Pamoja tujenge kanisa la Bwana (aaah!!)
Umoja ni nguvu,
Tukiwa pamoja twashinda (aaah!!)
Pamoja tujenge kanisa la Bwana (aaah!!)
Tunategemeana (aaaah)
Tusidharauliane (eeeeh)
Tuheshimiane (eeeeh)
Tupendane (eeeeh)
Tunategemeana (aaaah)
Tusidharauliane (eeeeh)
Tuheshimiane (eeeeh)
Tupendane (eeeeh)
Tutiane moyo na tushirikiana tuujenge mwili wa kristo!!!
Kiitikio]
Umoja ni nguvu,
Tukiwa pamoja twashinda (aaah!!)
Pamoja tujenge kanisa la Bwana (aaah!!)
Umoja ni nguvu,
Tukiwa pamoja twashinda (aaah!!)
Pamoja tujenge kanisa la Bwana (aaah!!)
Amen amen amen!!

More songs by Mwl. Listen to songs created by others
FROBITS