[male
vocals] (
Gentle
Ud
and
rhythmic
percussion
fade
in)
Twende
Mateka.
Wangu
kipenzi
jalia,
Leo
nakuandikia,
Kimya
kimenishindia,
Kulificha
hili
penzi.
Menishinda
kuzuia,
Huba
lilonifikia,
Nahofia
kuumia,
Mwishowe
n’
kate
pumzi.
Chonde
nipe
masikio,
Nikianza
na
pambio, ‘
Sijaribu
kula
mbio,
Ukanitwika
maudhi.
Ma’
na
nakosa
fahamu,
Tena
kubwa
yangu
hamu,
Kukushika
mnadhimu,
Kwa
bashasha
na
mapenzi.
Maungoyo
msichana,
Kila
ninapoyaona,
Moyo
wangu
wanikana,
Subira
kuipa
ngazi.
Myondoko
unayokwenda,
Mie
hali
yanishinda,
Moyo
mbiyo
wanidunda,
Nakuwa
jitu
chagizi.
Kidani
nakutunuku,
Kuifanya
tabaruku,
Huba
hili
silishuku,
Sitakufanya
ajizi.
Wazuri
ni
malaika,
Kwa
mola
wamesifika,
Nawe
kwangu
kadhalika,
Nimekupa
hiyo
hadhi.
Ewe
kwangu
mtukuka,
Kwao
wengi
walozuka,
Madaraja
umevuka,
Kwako
ninaweka
pozi.
Mahabani
nimefika,
Kooni
yamenifika,
Nyuma
kamwe
kugeuka,
Mwiko
huo
nauenzi.
Huba
hili
kulienzi,
Ni
wajibu
siyo
kazi, ‘
Takufanya
uwe
mwenzi,
Wa
faraja
na
maradhi.
Wanivuta
kwa
hisia,
Kufuata
yako
njia,
Mtima
umeridhia,
Uwe
wangu
mwandamizi.
Tamati
hapa
natua,
Mwisho
wa
hii
barua,
Wazo
niloligundua,
Twende
kwetu
kwa
wazazi.
Twandame
twende
Mateka,
Nawe
kijiji
tamka,
Nyumbani
ulikotoka,
Huko
tukapate
radhi.
Hili
jambo
ni
murua,
Baraka
kuzichukua,
Ni
adili
nilojua,
Katika
yangu
makuzi.
Mwishowe
unipe
tunda,
Kwa
shauku
ya
kupenda,
Na
moyo
ukaukanda,
Nisiwe
na
pingamizi.
Ndimi
wako
Mjamungu,
Nilotuma
hizi
fungu,
Kwako
wewe
Mbavuzangu,
Uliye
wangu
azizi.