Frobits
🎵 A song made on Frobits

Nitakuabudu Milele (Remix)

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

Chituz anafariji.
*ADUPE NENDA SALAMA KAKA.*
Machozi mazito na Moto yanatiririka,
Nikiitazama taswira ya picha yako Kaka Duplex umetutoka,
Umetuponyoka,
Umetuwacha walimu Kwa majonzi twahuzunika,
Duplex hili ni pigo tumebaki twaweweseka.
Adupe katupa mkono wa buriani
Adupe lala salama,
Msalimie rafikiyo Ododa,
Na somo wako Okumu wuod Nyakach Koguta.
Hatutasahau sauti yako Okumu,
Unapoenda mbele za hukumu,
Jua kifo twakishutumu,
Kwakuwa Kwa uchungu kimetudhulumu,
Adupe katupa mkono wa buriani
Adupe lala salama,
Msalimie rafikiyo Ododa,
Na somo wako Okumu wuod Nyakach Koguta
Kaka umeenda jongomeo,
Ijumaa nyeusi ya Leo,
Huzuni kuu Kwa familia, Wana na hata mkeo,
Adupe katupa mkono wa buriani,
Adupe lala salama,
Msalimie rafikiyo Ododa,
Na somo yako Okumu wuod Nyakach Koguta
Tuliandikwa siku na mwaka mmoja gange,
Tukafika upeo wa sarange,
Suruale zako za kimtindomtindo,
Kwa hakika zilitia fora Kwa vishindo,
Adupe katupa mkono wa buriani.
Adupe lala salama,
Msalimie rafikiyo Ododa,
Na somo yako Okumu wuod Nyakach Koguta
Wazazi,walimu na wanafunzi wa Kiswaro,
Ni kama umewawacha Kwa shimo lenye mitaro
Huzuni kuu imetanda kijiji cha Kiswaro....
Machozi Yao yanatiririka bila kupumzika
Adupe katupa mkono wa buriani
Adupe lala salama,
Msalimie rafikiyo Ododa,
Na somo yako Okumu wuod Nyakach Koguta
Adupe buriani
Okumu kwaheri
Adupe buriani
Okumu kwaheri.......

More songs by Owiti Listen to songs created by others
FROBITS