From Bakarani Mombasa to Morogoro Tanzania, family has come to celebrate with you our little darling
Miaka kumi na saba katika ndoa bila mtoto
Tukisubiri kwa subira na imani kubwa ya moto
Allah subhana wataala akatupa baraka ya kweli
Ilhamu ukazaliwa, tunu na faraji ya mwili
Leo ni harusi yako, chaguo la roho umepata
Nabiri mume wako, heri mnaenda kuifuata
Ilhamu na Nabiri, upendo ukae daima
Mwanzo wa maisha mapya, baraka za nchi nzima
Amani, furaha na upendo ziwajaze moyoni
Kutoka Hadija na Abdallah, baraka zenu zipokewe, one love
Sherehe na nderemo karibu ukumbini leo
Wageni waalikwa pongezi kwa huu msherehekeo
Mama Hadija chozi lanidondoka kwa furaha tele
Kuona mtoto wangu wa pekee akipiga hatua ya mbele
Allah awape umri mrefu na watoto wema daima
Mkaishi kwa amani, furaha isiyo na kikoma
Tunakupenda sana Ilhamu, mtoto wetu wa pekee
Nabiri na Ilhamu, jah bless ndoa yenu milele
One love, yeah, amani daima