Mambo vipi, Lightness...
Kipenzi cha roho yangu, eeh.
Sikia basi, ninaomba msamaha, eeh mamaa!
Nakumbuka ahadi zako mpenzi wangu
Ulisema hutotaka nisononeke
Ila leo hata salamu hunipi mwenzangu
Nilikuambia ni mtoto, sikutaka kukuudhi
Moyo wangu unaumia, nataka turudi
Lightness, tafadhali zungumza nami, eeh
Lightness, kipenzi cha roho yangu mimi
Nampenda sana yule anayejua siri zangu
Usiniache kwenye giza, rudi kwangu
Hata neno moja tu, litaponya moyo wangu
Kosa langu ninalijua, nimekiri leo
Kukosa sauti yako ni makubwa maumivu nayo
Ahadi yako ya furaha iko wapi sasa?
Upendo wetu wa dhati usiuache ukapotea kabisa
Nisamehe bure mpenzi, usinitupe gizani
Lightness, tafadhali zungumza nami, eeh
Lightness, kipenzi cha roho yangu mimi
Nampenda sana yule anayejua siri zangu
Usiniache kwenye giza, rudi kwangu
Hata neno moja tu, litaponya moyo wangu
Niambie nikufanyie nini mamaa sipendi kuwa hivi sipendi kulazimisha hisia zako najua kuna mtu unampenda sana ila mimi kahesi nina malengo ya dhatu kwako ...
Lightness wangu, nakupenda sana.
Usiniache hivi, sikatai sina mali sina cheo kikubwa ila nina malengo ya kukufikisha uendako...