Frobits
🎵 A song made on Frobits

Mungu Alimtuma Yona

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

Mungu alimtuma Yona
Mungu alimtuma Yona
Ili aende Ninawi, ili akahubiri, Neno la Mungu
Lakini Yona alikataa, kakimbilia Talishishi, akapenda Melikebuu kukwepa uso wa Mungu.
Meli ikakumbwa na dhorubaa (aah)
Yona akatoswa bahari (iih!)
Meli ikakumbwa na dhorubaa (aah)
Yona akatoswa bahari (iih!)
Hauwezi kukimbia uso wa Mungu, ukajificha asikuonee
Yona kamezwa na Samaki
Siku ya tatu katapikwa
Ukauona mkono wa Mungu
Karudi kuhubiri neno la Mungu
Yona kamezwa na Samaki
Siku ya tatu katapikwa
Ukauona mkono wa Mungu
Karudi kuhubiri neno la Mungu
Ndugu usikatae wito(ooh!)
Bwana anapokuita, inuka katende kazi nenda kafanye kazi ya Mungu
Eneza injili ya Yesu
Usidanganywe na shetani (iih!!)
Dunia itakumeza kisha yakutapika na mwishowe jehanamu milele
Yesu anakuita akupumzishe mizigo yako
Akusamehe dhambi zako uwe wake daima
Njoo kwake Yesu mponya yeye anakupenda
Toka ugenini ulipo
Hukk hakuna amani!!
Itikia wito wako wa mwanzo ulionao wa kumwimbia nyimbo za sifa
Mbona umeacha wito wako wa kwanza?
Rudi rudi rudi
Huko ugenini hupati amani
Njoo tumwimbie Mungu pamoja
Yeye atupendaye!!
Njoo njoo!!!

More songs by Mwl. Listen to songs created by others
FROBITS