Frobits
🎵 A song made on Frobits

Sebene Ya Ushindi (Remix)

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

Chriss Msaki Nasifu kuwa Daudi akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.
Basi Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalileta sanduku la Bwana kwa shangwe, na kwa sauti ya tarumbeta.
Ikawa, sanduku la Bwana lilipoingia mji wa Daudi Mikali, binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akiruka-ruka na kucheza mbele za Bwana; akamdharau moyoni mwake.
Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu.Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako, Nitaingia nyumbani mwako; Na kusujudu kwa kicho, Nikilielekea hekalu lako takatifu.
Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele. Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa
mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.
Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.

More songs by Man Listen to songs created by others
FROBITS