Blessings to the whole family
ARWA CHITU song.
Blessings to the whole family to have a blessed Day, be able to make ends meet.
BARAKA ZA RABUKA.
Ewe Mola,
Mbele zako twaja.
Tukiomba siku ya Leo na siku nyingine Zote.....uteremshe baraka Kwa yangu familia.
Neema zako zifike
Huruma yako ifike
Upendo wako ufike
Mapenzi yako yafike
Kila mmoja apate posho lake na Baraka ziwafinike.
BARAKA zako Rabuka.
Kwa kweli NI za kuaminika,
Mema yatatufika,
Mipaka yetu yatapanuka,
Mkonowe ukiteremka
Rabuka!
Tuma baraka.
Na jinalo litasifika
Tuepushie mabaya
Wanaotege mitego tawanya,
Njia zao finya,
Tutangulie Kwa njia,
Hali yetu pia
Utazame na Njema siha,
Wadogo wote na pia wakubwa,
Hekima itujae,
Shida tutatulie kwa wepesi wa akili na malaria ulltujaza,
Nguvu za kufanya KAZI Kwa ujuzi Mkuu,
Iwe mikono au miguu,
NI wewe ndio mpaji kutoka juu,
Si kazini,shuleni,hata uwanjani,
Mapato ya kila siku ujaze,
Ndoto zetu zitimize,
Magumu yenye kutu uyeyushe,
Ili yote yaishe,
BARAKA zako Rabuka.
Kwa kweli NI za kuaminika,
Mema yatatufika,
Mipaka yetu yatapanuka,
Mkonowe ukiteremka
Rabuka!
Tuma baraka.
Na jinalo litasifika.