Mapenzi yangu kwako, oh baby
Ni kama moto usiyozimika
Siku ya kwanza nilipokukuta umekaa kwa pozi la aina yake
Moyo wangu ukajua hii ni hadithi ya namna yake
Matendo yako yananifanya kila asubuhi niamke nikazisake usikimbie
Sikia kama ulimwengu umebadilika kwa ajili yako
Basi Macho yako yasione ya walimwengu
Sauti yako ni wimbo mzuri usinitoke kichwani mwangu nitakuimba mawio mpaka lizame, tukipata ridhiki siku tutafurahi kwa kinywaji laini huku tukikumbuka our memories first day we meet each other baby
Mapenzi yangu, kupenda kwangu
Kwa moyo wangu wote, haba na huba sita kufa
Mapenzi yangu, kwa ajili yako
Ni kama ndoto sitaki kuamka
Mapenzi yangu, oh how can I let you go baby
Kila mwendo wako unanirudisha nyumbani mapema
Kila jambo na wakati wake basi wewe ni saa hutoki mkononi mwangu nakucheck all the time hatuhitaji maneno mengi kwetu ni busu na furaha zaidi ya yote
Usije nisahau baby I will die
Nikumbuke kila saa kama mlokole na ibada
Umefika ndani ya moyo wangu, kutoka ni sawa na kupenya kwa sindano babygirl
Mapenzi yangu, mapenzi yangu
Kwa moyo wangu wote, haba na huba sita kufa
Mapenzi yangu, kwa ajili yako babygirl
Ni kama ndoto, sitaki kuamka
Mapenzi yangu, oh how can I let you go baby
Oh, nahitaji kuwa kando yako kila wakati kila siku usiwe kama watu fulani wasiopenda tufurahi
Kwa dunia, kwa miaka yote
Mapenzi haya ni kweli, tufurahie wakati wetu kipenzi changu
Ni mwanzo tu wa hadithi nzuri yangu na yako
Mapenzi yangu
Forever yours
Mapenzi yangu, ayee
Ni Mwarabu kwenye hii tena naimba mapenzi