Frobits
🎵 A song made on Frobits

Asante Baba

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

Asante baba, asantee, asante baba
Wewe ni Mungu, umenibariki na umenilinda
Wakati wote, shukrani zangu ni kwako
U mkuu sana baba, sifa na utukufu ni kwako
Zidisha fadhili zako baba, naomba neema
Rehema zako siku zote za uhai wangu
Asante baba, asante umenibariki mimi
Umebariki familia yangu, u mwema baba
U mwema nyakati zote, sifa na utukufu ni vyako
Asante baba, asante baba, asanteee!
Umekaa karibu, umesikia kila teso
Umeokoa roho yangu, umepatia moyo utulivu
Pendo lako halina mwisho, baraka zako ni majira yote
Naomba kila siku, neema na rehema zako
Asante baba, asante umenibariki mimi
Umebariki familia yangu, u mwema baba
U mwema nyakati zote, sifa na utukufu ni vyako
Asante baba, asante baba, asantee!
Sifa na utukufu ni vyako, baba
Mbingu na ardhi ni mali yako
Nani kama wewe baba
Ulinibeba nikiwa sijiwezi, nani kama wewe
Ukanijua ningali ni tumboni mwa mama, wewe ni Mungu
Ukuu wako wafanana na nini, Oooh baba
Hakuna kama wewe!
U Mkamilifu haswa, sifa na utukufu ni vyako
Asante, asante, asante baba
Asantee, Ooooh Asante Baba wa mababa
Asantee

More songs by Meja Listen to songs created by others
FROBITS