Maria mama yangu.
Wewe ni malkia wangu
Na mimi ndio mwanao Stanford
Leo nakuimbia Mamangu
Mama nakupenda sana
Moyo wangu umejaa upendo
Toka nije first day mpaka leo
Umekuwa furaha yangu
Kila siku namshukuru Mungu
Kwa kila tendo, kwa kila sala
Unanifanya niwe na furaha
Mama wangu, mama yetu pekee
Moyo wangu umelidhia kwako mama
Usiache mama, usiache kamwe
Wewe ni nuru yetu ya milele
Nakupenda sana mamaaaa
Wewe ni zawadi kutoka mbinguni
Nimekuona ukiteseka kwa ajili yetu
Lakini hukukata tamaa
Umenifundisha kuwa hodari
Umenifundisha kuamini
Machozi yako ni dhahabu
Sauti yako ni wimbo wa malaika
Mikono yako ni salama yangu
Upendo wako hauna mwisho
Mama wangu, mama wangu pekee
Moyo wangu umelidhia kwako mama
Usiache mama, usiache kamwe
Wewe ni nuru yangu milele
Nakupenda sana mamaaaa
Wewe ni zawadi kutoka mbinguni
Mungu akubariki mama
Akuzidishie nguvu
Akukinge na mabaya
Upendo wako hauna kifani
Mwanao Mercy,Samason wanakupenda
R.I.P kwa Dada yetu Upendo
R.I.P kwa jembe letu Aike
Tunamtukuza Mungu kwaajili yao
Mama wangu, mama wangu pekee
Moyo wangu umelidhia kwako mama
Usiache mama, usiache kamwe
Wewe ni nuru yangu milele
Nakupenda sana mamaaaa
Wewe ni zawadi kutoka mbinguni
Usiache mama, usiache kamwe
Nakupenda sana mama wangu
Mjukuu wako David anakupenda saaaaaana