Sir Nixy on this one...
Yo, manze... inauma sana.
Kila Father's Day mi hulia, yaani.
John, baba yangu... nakumiss sana.
Ulienda nikiwa mtoi wa miaka saba tu,
Ukaniacha kwa hii dunia, giza tupu.
Kila mara nikikumbuka sura yako napata machungu,
Nalia kwa kimya, nakuomba kwa Mungu.
Leo ni Father's Day, kila msee anajivinjari,
Wengine wako na madingo wao, wanajaa heri.
Mbona ulienda mapema, ukaniacha upweke?
Kumbukumbu zako moyoni, nazishika pekee.
Ningekuwa na wewe leo, Baba John,
Ningekununulia suti kali ya designer, uvae nikuone.
Tungekunywa mvinyo ya bei, tusherekee pamoja,
Nisikie upendo wa baba, roho ipate kupona.
Lakini unaondoka, unaniachia vilio,
Kila nikiwaza kuhusu wewe, machozi ndio kimbilio.
Maisha ya Kanairo bila wewe imekuwa ngumu,
Natamani ungaliona mwanao akitafuta hii ukumu.
Ningekupeleka out, tukule choma na marafiki,
Nikulindie heshima yako, bila hata dhiki.
Lakini sasa ni picha tu naangalia kwa ukuta,
Machozi yanadondoka, moyo wangu unajikuta.
Manze, inauma!
Ningekuwa na wewe leo, Baba John,
Ningekununulia suti kali ya designer, uvae nikuone.
Tungekunywa mvinyo ya bei, tusherekee pamoja,
Nisikie upendo wa baba, roho ipate kupona.
Lakini unaondoka, unaniachia vilio,
Kila nikiwaza kuhusu wewe, machozi ndio kimbilio.
Rest in peace, Baba John.
Sir Nixy amewacha machozi hapa...
Manze... tutapatana baadaye.
Ah, yo... peace.