Chituz!
Mapenzi Mwizi
Kuna gonjwa kuu duniani
Lishaua, linaua na linazidi kuua
Muhuni mkubwa,mwizi WA mioyo, mvunja ahadi,kichapo cha wote....,.......jina lake Mapenzi!
Mapenzi katugeuza washenzi
Jamani hili neno mapenzi
Kwa kweli nani Yuko na manual Yake?
Unasifiwa na kutungiwa tenzi
Kisha mwisho unawachwa Kwa Giza,
Mwili unakonda Sawa na pizza
Mipango yote inakatiza,
Badala ya sifa sasa u Sawa na Yai viza!
Ushapata visa ya kukonda kama ng'onda!
Kuna gonjwa kuu duniani
Lishaua, linaua na linazidi kuua
Muhuni mkubwa,mwizi WA mioyo, mvunja ahadi,kichapo cha wote....,.......jina lake Mapenzi!
Mapenzi katugeuza washenzi
Si walalahoi hata wenye mabenzi
Mapenzi yanawafanya washenzi
Haki wewe mapenzi
Si Nani ulimweka akachukua Kamba alipowachwa na Yule mrembo WA kikamba!?
Kuna gonjwa kuu duniani
Lishaua, linaua na linazidi kuua
Muhuni mkubwa,mwizi WA mioyo, mvunja ahadi,kichapo cha wote....,.......jina lake Mapenzi!
Mapenzi katugeuza washenzi
Mapenzi wewe!! huchagui msomi,mjuaji wala mshamba
Wote unawaramba mbele yako hawajawahi kutamba!
Wanabaki wakijaza vitambaa
Kwa jasho,makamasi kama wamevimba!
Kuna gonjwa kuu duniani
Lishaua, linaua na linazidi kuua
Muhuni mkubwa,mwizi WA mioyo, mvunja ahadi,kichapo cha wote....,.......jina lake Mapenzi!
Mapenzi katugeuza washenzi