MFANYIENI BWANA SHANGWE
Mfanyieni Bwana wetu Shangwe
Shangwe dunia yote
Mtumikieni Bwana, Bwana wetu kwa furaha
Njooni mbele zake Bwana, tena njoni kwa kuimba,
Jueni kwamba yeye Bwana, yeye ndiye Mungu wetu,
Ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake
Mfanyieni Bwana wetu Shangwe
Shangwe dunia yote.
Ndiye Bwana aliyetuumba
Na sisi tu watu wake
Sisi tu watu wake Bwana
Na kondoo wa Malisho yake
Ingieni Malangoni mwake
Ingieni kwa kushukuru
Nyuani mwake kwa kumsifu
Lihimidini Jina lake
Kwa kuwa Bwana ndiye Mwema
Rehema zake za milele.
Mfanyieni Bwana wetu Shangwe
Shangwe dunia yote
Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana, tumsifu Bwana Haleluya; x 2
Msifuni Mungu katika patakatifu pake, Msifuni Mungu katika anga la uweza wake
Msifuni Mungu kwa matendo yake makuu, Msifuni kwa Kadiri ya wingi wa ukuu wake,
Msifuni Mungu kwa mvumo wa baragumu, Msifuni Mungu kwa kinanda na kinubi,
Msifuni Mungu kwa matari na kucheza, Msifuni Mungu kwa zeze na filimbi
Msifuni Mungu kwa matoazi yaliayo, Msifuni kwa matoazi yavumayo sana,
Kila mwenye pumzi, amsifu Bwana, tumsifu Bwana Haleluya
Msifuni kwa matoazi yavumayo sana,
Kila mwenye pumzi, amsifu Bwana, tumsifu Bwana Haleluya