Frobits
🎵 A song made on Frobits

Yesu Kisu cha Dhambi (Remix)

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

*YESU KISU CHA DHAMBI.*
Utunzi WA Owiti ARWA CHITU
Mterehemezi mwenye kuteremsha, neema kubwa kubwa na ndogo ndogo,
Twajua hakuna aliye pamba,
Awe mfitini ama mwizi WA mashamba, na watu kuwaramba,
Hakuna anayeweza kutamba,hata aje na kubwa Kamba,
Mbele zako, hata aje Kwa Kali ndhumba,
Atajua fika kuwa wewe ndio Simba wa Masimba!
Mbele zako DHAMBI hazina ukiritimba,
Wewe utabaki kuwa Njamba,
Wewe ndio KISU cha Moto.........
YESU KISU cha DHAMBI,
Iwe kanisani,nyumbani,hospitalini ama za kijeshi kambi,
YESU KISU cha DHAMBI.
Tuna madoa yaliyokithiri,
Uchafu uliowazi na si Siri,
Walio majumbani na hata wanaosafiri,
Matendo yeti yakikafiri,
Yesu wewe ndio KISU cha Moto...
YESU KISU cha DHAMBI,
Iwe kanisani,nyumbani,hospitalini ama za kijeshi kambi,
YESU KISU cha DHAMBI.
Tuna mavunde na mvundo,
Yanukayo kama shombo,
Kwa hakika Yesu wewe NI sabuni kuliko ya vyombo,
Binadamu amekuwa chombo,
Chombo cha DHAMBI na mambo kombokombo,
YESU wewe ndio KISU cha Moto
YESU KISU cha DHAMBI,
Iwe kanisani,hekaluni, nyumbani,hospitalini ama za kijeshi kambi,
YESU KISU cha DHAMBI.
Pekee yetu Mterehemezi hatuwezi,
Bila wewe Yesu tuko Tu kama machizi,
Twafurahi tukiona damu ikichirizi,
Twajifunga mishanga ya kijini na mairizi,
Tu wageni WA waganga si Simbawanga si Potirizi,
YESU wewe ndio KISU cha Moto!
YESU KISU cha DHAMBI,
Iwe kanisani,nyumbani,hospitalini ama za kijeshi kambi,
YESU KISU cha DHAMBI.
YESU KISU cha DHAMBI!
Yesu KISU cha DHAMBI
Yesu Kisu cha DHAMBI.

More songs by Owiti Listen to songs created by others
FROBITS