Mr Dreezy
Someone wa somebody
Mmh, irudiwe
Siku ile, mpenzi wangu
Tulikutana siku moja tu
Mbona nakuwaza wewe tu
Bado nina kumbukumbu nyingi kuhusu wewe
Tena nina duku duku kama nipo mwenyewe
Itakuwa ngumu kuamini kama hauna mwingine
Itakuwa ngumu zaidi ukiwa nae niende kwingine
Sijui sana kuhusu tabia yako,
Lakini natamani iwe kama sura yako
Sitaki kuchambua mapito yako
Napaswa kutambua kwangu mchango wako
Ninazidi kukuona hata nikifumba macho,
Natamani nikugande zaidi ya kikulacho
Umeumbwa na aibu umekuzwa na stara,
Nisogeze karibu wasije kuiba kimasihala
Leo naomba Mungu anirudishie
Siku ile tena, mpenzi wangu
Irudiwe, siku ile tuliyokutana
Irudiwe, moyo wangu wataka tena
Nakumbuka kila neno, nakuwaza bila kikomo
Irudiwe mpenzi, nakuhitaji sana
Irudiwe, nakuhitaji sana
Siyo tu jina lako,
Ninakumbuka kila herufi
Kikubwa uwepo wako,
unaniimbisha kila sarufi
Sitafuti kiwanja nijenge,
Moyoni mwako ni pazuri nitaishi
Sitamani kuingizwa mkenge,
Na Vyakunukia vya wabovu wapishi
Siku tulokutana itabaki akilini,
Kama ni za mwizi ile ndo arobaini
Nitapunguza matumizi ya sabuni,
Na nitawapunguza wana na wahuni
Umeumbwa na aibu umekuzwa na stara
Nisogeze karibu wasije kuiba kimasihala
Leo naomba Mungu anirudishie
Siku ile tena, mpenzi wangu
Irudiwe, siku ile tuliyokutana
Irudiwe, moyo wangu wataka tena
Nakumbuka kila neno, nakuwaza bila kikomo
Irudiwe mpenzi, nakuhitaji sana
Irudiwe, nakuhitaji sana
Naimiss ile mida
Nakumiss wewe Frida
Mmh, irudiwe
Mpenzi wangu, irudiwe
Mr Dreezy
Someone wa somebody