Frobits
šŸŽµ A song made on Frobits

Moyo Umevunjika

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

Ayee... hii.... hiiƬ hiii
Life is harder maybe one day will be better than today
Asubuhi Kumekucha ni matumaini wenda itakuwa siku njema, Bila kujali ya jana mungu baba bariki leo iwe njema, kwa furaha na shangwe natoka home kutafuta kama ilivyo andikwa kula kwa jasho, mwamba najikaza mchana inapita jioni kiza kidogo mara paap simu za wana mwarabu njoo kuna show tunapatapata aloo sio poa mpaka jasho
Siwazi shida zangu because I'm okay natokea kitaa mvinyo unapigwa kicheko ni raha tu Kila mtu kafurahi... ni furaha nikiamini my day was better even though mifuko ni sufuri sio mbaya kesho nayo siku I thank God afya bomba let me enjoy my moment it's blessings to happy today hiii ooh....
Moyo unauma, maisha ni magumu mungu bariki
Bila wewe si kitu , hatua hazina nguvu na hustle zitafuta huzuni machoni one day
Nalia moyoni, usingizi umepotea kabisa
Eeh baba au siishi kukupendeza kama wale, maisha ni magumu, ufukara unatesa imani ni wewe pekee (mmmh nifundishe kunyamaza yawalimwengu ni mazito)
Marafiki wananiambia nitapona tu
Lakini jeraha hili ni kama kidonda kuchomwa sindano, kwenye lile shangwe ghafla furaha ikawa karaha, kukosa pesa ukiongea mbele yao unaleta fujo, aisee tutafute pesa hata salamu ni kero wasipo kufahamu, usinipe tano unanijua wewe? Kwa huzuni mikono chini Tabasamu la uongo pembeni naketi maswali ni mengi ila let's peace take place mwarabu wewe ni nani kwani? (mmmh nifundishe kunyamaza yawalimwengu ni mazito)
Siku inaisha kwa majonzi kama yatima kumbe ni waja na mambo yao, hatuombi mabaya ila tubariki kama wao sisi wote waja wako na tunapiga kazi kama wao levels isiwe mipaka salamu kwetu ni jadi waTz hata wale strangers one love ndio utu wa mwafrika hiiii
Moyo unauma, maisha ni magumu mungu bariki
Bila wewe si kitu , hatua hazina nguvu na hustle zitafuta huzuni machoni one day
Nalia moyoni, usingizi umepotea kabisa
Eeh baba au siishi kukupendeza kama wale, maisha ni magumu, ufukara unatesa imani ni wewe pekee (mmmh nifundishe kunyamaza yawalimwengu ni mazito)
Ayee... hiiii..hiii..polepole tutafika safari ya mafanikio ni ndefu binadamu tuna mengi nifundishe kunyamaza yawalimwengu ni mazito papa God
Ni Mwarabu kwenye hii tena

More songs by Bonny Listen to songs created by others
FROBITS