Hallelujah! Asante Bwana kwa watoto hawa.
Senye Junior School, Grade Nine Winners!
Kazi yangu ya ualimu ni baraka kuu
Mungu amenipa zawadi kutoka juu
Wanafunzi wangu nyinyi ni washindi kweli
Upendo wenu unanijenga kila asubuhi
Mnanipa nguvu ya kusonga mbele
Grade Nine Winners wa Senye Junior School
Nawapenda sana, nawaombea kwa Mungu
Upendo wenu unanipa matumaini mapya
Mungu awabariki, awafungulie njia
Yesu awatunze daima
Kila asubuhi nikiwaona darasani
Moyo wangu unajaa furaha na amani
Mwalimu wenu najivunia ninyi sana
Tunasimama imara kwa nguvu za Bwana
Munajenga maisha yangu kwa upendo wenu
Grade Nine Winners wa Senye Junior School
Nawapenda sana, nawaombea kwa Mungu
Upendo wenu unanipa matumaini mapya
Mungu awabariki, awafungulie njia
Yesu awatunze daima
Nidhamu yenu ya juu itawapeleka mbali,kuamka kwenu asubuhi kutazaa matunda.Naomba mungu awafungulie njia wazazi wenu,naitaji yenu yetimie.mimi mwalimu Nyamongo nawapenda kwa moyo wangu wote.
Waheshimu wakubwa kwa wadogo,waswahili walisema heshima Si utumwa.wapende walimu wenu bila kupagua,mkifanya hivyo mtafaulu
Asante Yesu, bariki wanafunzi wangu.
Amen, hallelujah, amina!