TUMEAGIZWA UPENDO
Tumeagizwa upendo, upendo uwe ndani ya mioyo yetu.
Kama vile Mungu alivyo tupenda sisi tangu kule mwanzo.
Tumpende Bwana Mungu wetu, kwa moyo na akili zetu
Tuwapende na jirani kama tujipendavyo hizo ndizo amri kuu kwetu.
Tuwapende na jirani kama tujipendavyo hizo ndizo amri kuu kwetu!
Lakini sivyo tufanyavyo wanadamu, katika maisha yetu kila siku
Twachukiana sisi kwa sisi duniani,
Upendo kati ya ndugu na ndugu umetoweka
sivyo tufanyavyo wanadamu, katika maisha yetu kila siku
Twachukiana sisi kwa sisi duniani,
Upendo kati ya ndugu na ndugu umetoweka
Wakristo tumeitwa tusaidiane katika shida na raha za duniani
Mungu anapendezwa ndugu wakiwa pamoja kwa upendo furaha na amani
Maisha yetu yamejengwa kwa pendo la Mungu
Upendo ukiwepo unasitiri wingi wa dhambi
Huo upendo
Huvumilia yote
Huo upendo
Hauhusudu
Huo upendo
Hauhesabu mabaya
Huo upendo
Haujivuni
Huo upendo hautakabari na wala hutafuti mambo yake wenyewe...
Ndugu tupendane kwa upendo wa Mungu!!
Tunawezaje kusema kwamba twampenda Mungu tusiyemuona
Lakini ndugu na majirani tuishio siku zote pamoja hatupendani
Neno la Mungu linasema huo ni unafiki!!
Maisha yetu yamejengwa kwa pendo la Mungu
Upendo ukiwepo unasitiri wingi wa dhambi
Huo upendo
Huvumilia yote
Huo upendo
Hauhusudu
Huo upendo
Hauhesabu mabaya
Huo upendo
Haujivuni
Huo upendo hautakabari na wala hutafuti mambo yake wenyewe...
Ndugu tupendane kwa upendo wa Mungu!!