Roho yangu na ikusifu Bwana daima
Nikusifu, nikusifu, daima
Mimi Emanuel, nasema neema zako hakika ni za milele
Fadhili zako haziwezi kuhesabiwa, rehema zako hudumu
Hajawai tokea kama wewe, hajatokea, hatatokea
Katika raha zangu, katika taabu, hukuniacha, ayee wewe ni Mkuu! Wewe ni Mkuu!
Umekuwa nami, baba yangu, bwana wangu kila wakati umekuwa nami
Hakika wewe ndiye mwamba salama, mwamba Imara! Mwamba salama!
Kwanini nisikusifu, kwanini nisikushukuru, Asantee Baba!
Daima nikusifu Bwana (nikusifu, nikusifu)
Nishangilie kila wakati (tena na tena)
Baraka zako, rehema zako
Zaidi ya nyumba, zaidi ya mali
Daima nikusifu Bwana (eeh baba!)
Hakika wewe ni Bwana, hakika wewe ni bwana!
Katika raha zangu, katika taabu hukuniacha
Wewe ndio nguvu yangu, wewe ndio furaha yangu
Hakika wewe ndiye mwamba salama
Kwanini nisikushangilie, kwanini nisikushukuru
Fadhili zako na neema, asante sana bwana
Mimi Emanuel, Mimi na Familia yangu ya Tarimo tunakusifu
Tunakumbuka, tunakushukuru, tunakushangilia
Daima nikusifu Bwana (nikusifu, nikusifu)
Nishangilie kila saa (tena na tena)
Baraka zako, rehema zako
Zaidi ya nyumba, zaidi ya mali
Daima nikusifu Bwana (ayee baba!)
Hakika wewe ni Bwana, hakika wewe ni bwana
Roho yangu na ikusifu daima
Daima, daima, hakika wewe ni Bwana
Asante sana, asante sana, bwana