[male
vocals] (
Taarab
style
oud
intro
with
light
percussion)
PENZI
LA
MAMA β
Naanza
kutakalamu,
kulisifia
penzi,
la
mama
alonilea
Nalinadi
kwa
nudhumu,
nayo
ndefu
simulizi,
wimbo
ninalitungia
Huba
ninaliheshimu,
tena
bila
ya
ajizi,
shime
nimejionea
Sijawa
mwendawazimu,
na
bichwa
halina
ganzi,
hilino
kulitambua. β
Swali
linanitekenya,
layumbayumba
kichwani, β
nani
mfano
wa
mama?β
Najikusanyakusanya,
silali
usingizini,
ruiya
zinanikwama β
Malaika
wanikanya,
ni
mwiko
yao
maoni,
mfanowe
kusakama
Ziraili
anionya,
nikuweke
fuadini,
maisha
hadi
kiama. β
Nafasi
ya
kwake
mama,
siyo
mithili
ya
jua,
ishikwayo
na
mbaβ
mwezi
Au
jua
likizama,
nyota
nazo
huchanua,
hutoa
yake
miyonzi
Ni
kiumbe
muadhama,
malezi
anayajua,
tangia
enzi
na
enzi
Mimbarini
nasimama,
nikikuombea
dua, β
sishikwe
na
angamizi. β
Niko
kando
ufukweni,
pepo
za
jozi
kwa
jozi,
zavuma
kwa
utulivu
Nakuwaza
muhisani,
maonyo
yako
ya
wazi,
yaso
shari
na
uovu
Jasho
nalowa
mwilini,
ninagubikwa
na
chozi,
siyo
kwa
penzi
la
wivu
Ni
rejea
za
zamani,
kumbukizi
za
malezi,
yako
mama
muangavu. β
Nikifanya
marejeo,
zama
zangu
utotoni,
mamangu
alinitonya
Akaningβ
ata
sikio,
na
kunitomasa
mboni,
mabaya
akanionya
Akanipa
mwelekeo,
lipi
bora
maishani,
na
baya
akanikanya
Kisa
cha
hili
pambio,
kuliweka
kitabuni,
wenzangu
mpate
ona β
Sina
maono
hafifu,
macho
yaliyo
dhoofu,
nisiyaone
mapenzi
Na
silewi
mkangafu,
niwe
mla
nyamamfu,
nikajitia
makuzi
Penzilo
ni
adilifu,
kwa
mapana
na
marefu, β
talipia
simulizi
Mama
u
mja
nadhifu,
wa
karama
afuafu,
kwa
malezi
na
ujuzi. β
Penzi
la
mama
bahari,
ichukuwayo
viumbe,
majini
na
wanadama
Livunjalo
majabali,
lisiache
hata
chembe,
mkembe
yakimwandama
Penzi
la
mama
johari,
kulibeza
usiambe,
utakufa
na
kuzama
Penzi
lishike
ngangari,
lishike
na
usiyumbe,
ni
dira
kuitizama. β
Mama
ni
nguzo
imara,
iliyozamishwa
chini,
kwa
mapenzi
ya
Moliwa
Ni
mpaji
wa
nusura,
atoa
nyingi
auni,
tabu
ukielemewa
Kwetu
hii
ni
tijara,
tuishike
mikononi,
aula
ungatambuwa
Mama
hana
taathira,
mfano
wake
ni
nani,
kichwani
kunizuzuwa.