Frobits
🎵 A song made on Frobits

Jemima Rudi Nyumbani (Remix)

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

Sir Nixy,
Hii ni barua ya husuni ya joseph sibora kwa mke wake Jemima simiyu,inaanza na kusema,
Jemima....mke wangu...
Ni mimi mumeo, sibora
Nyumba haina amani tangu uondoke,upweke unaniua huku...
Najua Cathy na Jemy kila siku wanakuuliza,Baba yuko wapi?
Tafadhali sikiliza kilio cha moyo wangu...
Nyumba imepoa,ukuta unanitazama
Kila kona ya kitanda,ina maswali Jemima
Upweke umekua blanket langu la usiku
Mawazo yanitesa,nakosa usingizi sasa
Nami mumeo sibora,nimebaki gofu la mtu
Namiss kicheko chako,namiss mapenzi yako ya dhati
Jemima rudi nyumbani,mbona umenitupa gizani?
Tuishi kwa pamoja,tulee watoto wetu kwa amani
Ni nini kilichokubadilisha ghafla ukasahau mapenzi?
Ukaziacha wapi ahadi zetu tulizozienzi?
Ni nini nilichokufanyia kisichokuwa na msamaha?
Hadi umechukia nyumba yetu,baada ya kupata kazi na furaha?
Cathy na Jemy, nikiwafikiria,machozi yananilenga
Nawatamani kuwaona tukicheka sote,mimi na wewe na watoto wetu
Kazi imekua ukuta,imekutenga na mumeo
Najua mimi si mkamilifu,mapungufu yangu nayajua
Kama nilikukwaza nisamehe,usivunje kiapo chetu
Rudi tufute haya machozi,rudi tupate faraja
Jemima rudi nyumbani,mbona umenitupa gizani?
Tuishi kwa pamoja,tulee watoto wetu kwa amani
Ni nini kilichokubadilisha ghafla ukasahau mapenzi?
Ukaziacha wapi ahadi zetu tulizozienzi?
Ni nini nilichokufanyia kisichokuwa na msamaha?
Hadi umechukia nyumba yetu baada ya kupata kazi na furaha?
Joseph Sibora mumeo,nalia...
Cathy na Jemy wananihitaji mimi baba yao...
Mlango uko wazi,rudi nyumbani Jemima...
Nisamehe...rudi tulee damu yetu..

More songs by Sir Listen to songs created by others
FROBITS