Ama kweli kuna watu na viatu,
Na Kuna watu Wana roho za chatu,
Sikujua kama jemq langu kwa mtu mwingine ni dhambi, e bwana kwa ni Kuna ubaya gani katika hili?
Umeacha Wallet yako wazi na ina shilingi elfu hamsini, mimi nikatoa shilingi elfu kumi tu unaanza kubuutia mwizi ebu acha robo mbaya.
Umenunua shamba la ekari kumi, mimi nikajimegea eka moja na kulima unaanza kunishikia panga ebu acha roho mbaya.
Umenunua gari zuri kwa jasho lako mimi nakuomba lift unaninyima ebu acha roho mbaya.
Umefungua mgahawa mzuri unapika chakula kizuri mimi kama rafiki yako nakuomba niwe nakula bure unakataa ebu acha roho mbaya usiye na haya.
Umeoa mke wa kwanza tukafurahia pamoja ,umeoa mke wa pili unang'ang'ania na wa kwanza wakati unajua sisi rafiki zako wote singo daaah acha roho mbaya kijana..
Ukiacha roho mbaya utafika mbali sana wallah wabinlahi.