Ayee Paulina
(Mpenzi wangu...)
Gitaa inalia kwa utamu
Asante kwa mapenzi yako Paulina
Kama yungi yungi katikati ya miiba
Ndivyo alivyo mpenzi wangu katikati ya wanawali
Tazama jinsi ulivyo mzuri Paulina mke wangu
Umeiba moyo wangu mpenzi kwa mtupo mmoja wa macho yako
Malkia wangu wa nguvu, nakupenda sana Bi Randiki
Tutaishi pamoja, tulee watoto kwa upendo
Tu enjoy maisha ndani ya Bwana
Aliye nionyesha wewe
Mimi penda wewe Sana jaber
Tabasamu lako linaponya majeraha yote
Kwenye mikono yako napata amani tele
Uzuri wako hauna mfano duniani
Wewe ni zawadi yangu kutoka kwa Mungu
Malkia wangu wa nguvu, nakupenda sana Paulina
Tutaishi pamoja, leo na kesho kutwa
Sauti yako tamu kama asali ya nyuki
Hadi mwisho wa dunia...
Yungi yungi wangu Paulina...
Nakupenda, mke wangu Bi Randiki
Raha yangu kupendana na wewe Raha tu
(Gitaa inapotea taratibu...)
(Ayee, my queen!)