Nimeona pendo lako kuu Yesu
Unanipenda upendo wa kweli nami nakupenda
Ulinifia msalabani pendo la namna gani
Upendo wa juu Yesu wangu
Ninaahidi kukupenda daima na kukutumikia
Asante Yesu kwa pendo lako
Pendo lako la ajabu sana
Huangalii tajiri wala maskini
Mrefu wala mfupi, mweusi wala mweupe
Wote unatupenda upendo wa ajabu
Asante Yesu kwa pendo lako
Wewe ni baba wa yatima na mume wa wajane
Tena unawafariji waghane
Yesu wewe utukuzwe daima
Pendo lako la ajabu Yesu wangu
I need you to compose this song