[male vocals] SAMAHANI
MPENZI.
Yalaiti
samahani,
kwa
vyangu
hivi
viliyo
Kukuweka
mtimani,
na
mengine
nikupayo
Nikazama
mahabani,
mahaba
kwako
ambayo
Hayazami
akilini,
usinijali
kwa
hayo.
Nisamehe
wahubani,
kwa
kuwa
langu
chaguo
Ni
kudura
za
manani,
siyo
langu
pendeleo
Tafadhali
sitarani,
moyo
wangu
upe
nguo
Niafiki
wangu
nyuni,
chozi
lifike
kituo.
Mwenzio
nipo
kizani,
nimepigwa
na
ukungu
Yamenifika
kooni,
makali
yake
machungu
Zigo
haliwezekani,
unituwe
nyuni
wangu
Kuishi
haiwezekani,
nikikosa
lako
fungu.
Mbele
nendako
sioni,
ja
wasemavyo
wahenga
Pendo
'kikaa
moyoni,
mtu
huzuka
mjinga
Ya
mbele
kamwe
haoni,
macho
yake
hujifunga
Tena
huwa
punguwani,
asosikia
waganga.