Frobits
🎵 A song made on Frobits

Mzee Konyezo (Remix)

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

Chituz,
Na Afrobit
*NISHIKE MKONO BWANA*
Nikiwa katika vita vikali,
Yanayoonekana hakuna ushindi awali,
Iwe ni mipangilio ama Kwa ajali,
YESU naomba unijali,
Jinsi ulivyomshindia Daudi dhidi ya lile Jitu Goliathi,
Nami pia nipe ushindi.
Nishike mkono Bwana, uniongoze Kwa safari Zote.
Mapito ni mengi
Vikwazo ni vingi
Maadui ni wengi
Ukame ni mwingi
Pesa ni chache-Matumizi ni mengi.
Bila wewe Yesu hakuna ushindi.
Na wakati vicheko vimezidi,
Jinsi siwezi kujifungua,
Kupata nami mtoto wa kunisumbua,
Jinsi ulivyomfaa Sarah,
Akapata yule karibu atolewe kafara,
Nishike mkono Bwana.
Mapito ni mengi
Vikwazo ni vingi
Maadui ni wengi
Ukame ni mwingi
Pesa ni chache-Matumizi ni mengi.
Bila wewe Yesu hakuna ushindi
Wakati mawazo yamefika mwisho,
Ukuta nimegonga, sina uhakikisho,
Ni kifo macho yamenikodolea,
Na siwezi kuogelea,
Jinsi ulivyowavukisha
Wana wa Israeli kuvuka bahari ya Shame,
Nami pia nivukishe
Shida zinihame,
Nishike mkono Bwana
Mapito ni mengi
Vikwazo ni vingi
Maadui ni wengi
Ukame ni mwingi
Pesa ni chache-Matumizi ni mengi.
Bila wewe Yesu hakuna ushindi
Wakati magonjwa yamenilemea,
Navamiwa hadi na vimelea,
Sehemu zote za mwili,
Si mtima, maini,mapafu na akili,
Mwili wote umechoka.....
Jinsi ulivyowaponya kina Bartimaus,
vipofu,viwete na wenye akili razini,
Niponye hata kabla sijafika hospitalini,
Niponye dhidi ya makali yoyote yale ya magonjwa.
Nishike mkono Bwana.
Mapito ni mengi
Vikwazo ni vingi
Maadui ni wengi
Ukame ni mwingi
Pesa ni chache-Matumizi ni mengi.
Bila wewe Yesu hakuna ushindi

More songs by Owiti Listen to songs created by others
FROBITS