Mr Dreezy someone wa somebody
Leah, Leah wangu
Mpenzi kutoka Chuga
Ah ah!
Nimekuona Leah, umeniangaza
Mrembo wa Chuga, moyo wangu unadunda sababu ya wewe
Nina kila sababu ya kujivunia uwepo wako katika maisha yangu
Wewe ni tafsiri ya neno uzuri usiondoke upande wangu
Najua tupo mbali lakini upo karibu sana moyoni mwangu
kila dakika ni ya thamani kwangu kwa sababu umekubali kuwa wangu
Nitakupenda nitakuheshimu na nitajitahidi Kukutunza na kukulinda kama mboni zangu
Maisha hayatakuwa na maana kama wewe hautakuwa sehemu ya hayo maisha
Kukutana na wewe ilikuwa ni bahati lakini kuendelea kuwa na wewe kama wapenzi ni faradhi
“Leah wangu una maana kubwa sana maishani mwangu”
“Leah wangu Nina kila sababu ya kusema wewe ni bahati yangu”
Natamani hata nibuni namna mpya ya kukuonesha upendo
Ili tu usije choka kunipenda ukapunguza mwendo
Malengo yangu hayatalenga chochote kama siyo kuishi na wewe
Ukiondoka hautoacha pengo bali ntafika ukingoni bila wewe
Usijebadili mtazamo wako juu yangu
Maana wako msimamo ndo furaha kwangu
Jitulize kwani yadunia yote yanapita
Ila wewe kwangu utakaa daima hata kwa vita
“Leah wangu una maana kubwa sana maishani mwangu”
“Leah wangu Nina kila sababu ya kusema wewe ni bahati yangu”
Mr Dreezy
Space Music