Ni mwarabu kwenye hii tena naimba eeh!
Asante Mungu, asante sana
Huu uhai ni zawadi yako
Ninaamka kila asubuhi kwa furaha
Kwa sababu roho yangu iko sawa kwa imani
Macho yangu yanatazama dunia hii
Kama zawadi kubwa sana
Huu uhai si kwa bahati
Ni kwa neema yako ya kila siku
Ninajua kuwa umeniandika
Katika kitabu cha uzima maisha yangu ni wewe, nijalie kuepuka kiburi cha uzima eeh Mungu baba
Kuomba na kuombea kheri wengine iwe sehemu ya maisha yangu japo kisasi ni haki tujalie amani eeh baba
Asante Mungu, asante sana
Kwa huu uhai, kwa kila saa
Huu uhai ni zawadi na upendo
Asante Mungu, dunia ni njia
Nakuomba, kuendelea kutupa neema
Asante sana, asante Mungu
Kila pumzi kwa giza
Kila alfajiri kwa anga angavu
Kila pumzi, na moyo wangu
Unakumbuka maandiko yako baba God
Wazazi, marafiki, na kila mtu
Wanastaajaabu kwa furaha uwepo wako
Ninajua kuwa umepanga njia yangu iwe nyeupe
Kila hatua, kila siku, kila mwaka ameen
Omo, huu uhai ni baraka!
Mungu atubariki sote
Tuwende pamoja kwa shukrani
Kwa baraka za kila saa na dakika maana dunia ina mengi baba
Asante Mungu, asante sana
Kwa huu uhai, kwa kila saa
Huu uhai ni baraka na upendo
Asante Mungu, dunia njia
Nakuomba, kuendelea kutupa neema
Asante sana, asante Mungu
Tupo Hai leo sio eti ni wajanja ni kibali na neema japo ipo siku tutaiacha Dunia
Bariki wale wote tunaomini katika wewe bila kujali dini
Kila kitu in this world tunaacha ila tusiache kuishi kwa upendo
Asante Mungu, asante sana
Huu uhai, huu uhai
Asante, asante, asante Mungu
Gospel time now Asante
God is good all the time