(Sauti ya kiume): Mungu wangu, pokea shukrani zetu...
(Sauti ya kike): Tunawakumbuka wapendwa wetu walio tangulia mbele ya haki...
Tunawakumbuka wazee wetu, wana wa Mayala
Sayi Milaba, Nila Mgata, Yohana Goleha
Pamoja na Maria Sumayi, uliwapa pumzi
Walijenga misingi, walitupa mwongozo wa maisha
Upendo wao, waliuishi kwa matendo makuu
Walijadiliana, migogoro wakaitatua kwa hekima
Ee Mungu wetu, wajalie pumziko la milele
Tunawakumbuka kwa machozi na upendo mkuu
Milaba, Goleha, Ncheye, wapendwa wote
Tutawaenzi daima, katika mioyo yetu
Tunawakumbuka Elias, Ndongo na Elizabeth
Nsungulwa, Mzee Ncheye, na Mzee Ndela pia
Monica Silya, mama yetu, shangazi yetu mpendwa
Masunga, Stephano, Sita na Buyegi
Tabu, Mgosha, Lengwa, Milembe na Ng'wanadoto
Nafsi zao zipumzike, kwa amani ya mbinguni
Ee Mungu wetu, wajalie pumziko la milele
Tunawakumbuka kwa machozi na upendo mkuu
Milaba, Goleha, Ncheye, wapendwa wote
Tutawaenzi daima, katika mioyo yetu
(Sauti ya kike): Ee Mungu tutunzie wazee wetu waliobaki
(Sauti ya kiume): Mabula, Saweli, Mbilize, Silya na Salime
(Sauti ya kike): Mama George, Sundi, Mashaka na Gachimu
(Sauti ya kiume): Mayange, Monga, tunawaombea baraka
Ee Mungu wetu, wajalie pumziko la milele
Tunawakumbuka kwa machozi na upendo mkuu
Milaba, Goleha, Ncheye, wapendwa wote
Tutawaenzi daima, katika mioyo yetu
(Sauti ya kike): Tunawakumbuka...
(Sauti ya kiume): Tutaishi kwa hekima mliyotufundisha...
(Wote): Pumzikeni kwa amani, tutakutana tena...
Milaba Ng'wanasilya.