*YESU KISU CHA DHAMBI.*
Utunzi WA Owiti ARWA CHITU
Mterehemezi mwenye kuteremsha, neema kubwa kubwa na ndogo ndogo,
Twajua hakuna aliye pamba,
Awe mfitini ama mwizi WA mashamba,
Hakuna anayeweza kutamba,
Mbele zako, hata aje Kwa Kali ndhumba,
Mbele zako DHAMBI hazina ukiritimba,
Wewe utabaki kuwa Njamba,
Wewe ndio KISU cha Moto.........
YESU KISU cha DHAMBI,
Iwe kanisani,nyumbani,hospitalini ama za kijeshi kambi,
YESU KISU cha DHAMBI.
Tuna madoa yaliyokithiri,
Uchafu uliowazi na si Siri,
Walio majumbani na hata wanaosafiri,
Matendo yeti yakikafiri,
Yesu wewe ndio mkuki WA Moto...
YESU KISU cha DHAMBI,
Iwe kanisani,nyumbani,hospitalini ama za kijeshi kambi,
YESU KISU cha DHAMBI.
Tuna mavunde na mvundo,
Yanukayo kama shombo,
Kwa hakika Yesu wewe NI sabuni kuliko ya vyombo,
Binadamu amekuwa chombo,
Chombo cha DHAMBI na mambo kombokombo,
YESU wewe NI mshale wa Moto
YESU KISU cha DHAMBI,
Iwe kanisani,hekaluni, nyumbani,hospitalini ama za kijeshi kambi,
YESU KISU cha DHAMBI.
YESU KISU cha DHAMBI,
Iwe kanisani,nyumbani,hospitalini ama za kijeshi kambi,
YESU KISU cha DHAMBI.
YESU KISU cha DHAMBI!
Yesu KISU cha DHAMBI
Yesu Kisu cha DHAMBI.