Ah ah! Milka, malkia wangu!
Twende, twende! Bongo!
Mara ya kwanza tulipo kutana mpenzi,
Hakuna alie amini kama tutapendana,
Wengi walisema sisi ni wageni wa jiji,
Waliamini tutaachana kwa dakika chache tu,
Lakini sasa tazama tunavyong'aa,
Upendo wetu unazidi kuwa tamu kama asali,
Siwezi kuwaza maisha bila wewe,
Milka wewe ndio furaha ya moyo wangu.
Milka, mpenzi wangu wa dhahabu,
Milka, mama watoto wangu wa baadaye,
Namshukuru sana Maulana kwa kutupa nguvu,
Nguvu ya kuvumiliana katika mapenzi,
Sizani kama kuna mtu atakuja tugombanisha,
Kwa sababu penzi letu limejengwa na Mungu.
Watu wanasema mengi mitaani,
Wanatamani kuona tunavyotengana,
Lakini hawajui siri ya mioyo yetu,
Siri ya kuvumiliana kila iitwapo leo,
Ninakupenda Milka, nakupenda sana,
Sauti yako inatuliza dhoruba za moyo,
Ukiwa karibu nami, naona amani,
Milka, wewe ni zawadi yangu ya kipekee.
Milka, mpenzi wangu wa dhahabu,
Milka, mama watoto wangu wa baadaye,
Namshukuru sana Maulana kwa kutupa nguvu,
Nguvu ya kuvumiliana katika mapenzi,
Sizani kama kuna mtu atakuja tugombanisha,
Kwa sababu penzi letu limejengwa na Mungu.
Kila uchao, namuomba Mola,
Akulinde, akuweke salama,
Isije ikatokea kitu cha kututenganisha,
Maana wewe ni nuru ya macho yangu,
Milka, penzi lako ni dawa ya moyo.
Tutaendelea kupendana daima,
Tutaendelea kushikana mikono,
Iwe Dar au popote pale tutakapokuwa,
Upendo wetu utabaki kuwa mfano bora,
Milka, wewe ni malkia wangu wa moyo,
Nakupenda leo, kesho na hata milele.
Milka, mpenzi wangu wa dhahabu,
Milka, mama watoto wangu wa baadaye,
Namshukuru sana Maulana kwa kutupa nguvu,
Nguvu ya kuvumiliana katika mapenzi,
Sizani kama kuna mtu atakuja tugombanisha,
Kwa sababu penzi letu limejengwa na Mungu.
Milka, mpenzi wangu, poa sana,
Twende, twende, ni wewe tu,
Milka, ah ah, malkia wangu,
Nakupenda milele, Milka.