Hallelujah, Hallelujah! Yesu ni Bwana, amen
Rafiki wa kweli, namwamini Yeye tu, amen
Nikiwa na Yesu mimi ni shujaa
Kama ni kusema maneno yote wameshasema
Maneno yao yaliyowafurahisha walisema
Ila hawakuchunguza wajue ukweli
Walinisema mambo ya uongo yasiyofaa, oh Lord
Hawakujali kiwango cha maumivu ya roho yangu
Wanadamu hao, waongo wanadamu
Viumbe wanadamu vyasikitisha moyo wangu
Wanadamu hao, waongo wanadamu
Lakini Mungu mtetezi wa wanyonge atanitetea
Nakataana na maneno yenu, navunja baraza zenu
Nasambaratisha vikao vyenu vya umbea kwa jina la Yesu
Mabaya mlionitakia iwarudie kwa jina la Yesu
Kusudi mniangamize sasa msambaratishwe
Mnyamazishwe, mfedheshwe, mnyenyekezwe
Kwa jina la Yesu, Amen, Amen!