Frobits
🎵 A song made on Frobits

Sauti ya Sifa

0:000:00
Download
Reply with a song
Lyrics

Solo ya kike:
Nimekuandikia kijana kwani una nguvu za kumshinda mwovu,
Nguvu zako ziko wapi kaka? mbona unakatishwa tamaa mapema
Nguvu zako ziko wapi dada? mbona warudi nyuma kila wakati,
Yesu Kristo anaulizaaaa, talanta uliyopewa umeweka wapi?
Je umeizalisha? ili ajapo apate faida,usiizike chini bora uiweke kwa watoa riba ajapo Bwana asipate hasaraaaaa, inuka utendeee maana shughuli hii ni yako wewe,
Simama, jitie ujasiri majaribu ni ya kitambo kidogoooo
Chorus
Kijana inuuuukaaaa, tenda kazi ya Bwana,
Nafasi uliyopewa si ya kuipoteza inagharama,
Kanisa linajengwa na weweeee
Kanisa linajengwa na mimiiii
Kanisa linajengwa na sisi vijana
Tuweke bidiiii.
Solo
Unaitwaaaa ndugu yangu, isifanye moyo mgumu,
Leo ni yako na muda ni sasa ila jua kesho ni ya Mungu.
Nafasi unayo bado akusubiri, Hakuna mwisho wa rehema zake ni mpya kila siku asubuhi Mwangaza wake unajaza moyo
Rehema zake ni za mileleeee, rudi sasa nafasi unayo usifanye moyo mgumu weeeee kijana weeeweee
Chorus
Kijana inuuuukaaaa, tenda kazi ya Bwana,
Nafasi uliyopewa si ya kuipoteza inagharama,
Kanisa linajengwa na weweeee
Kanisa linajengwa na mimiiii
Kanisa linajengwa na sisi vijana
Tuweke bidiiii.
_Kutumia maneno yako kama yalivyo — gusa *Hariri maneno* ili kurekebisha._

More songs by emma Listen to songs created by others
FROBITS