Simama imara, tetea imani yako,
Simama tangaza injili ya Yesu.
Simama imara, eneza upendo wa Yesu,
Ya kwamba ni Bwana naye anaokoa!
Kijana kipofu tangu kuzaliwa kwake,
Alipoponywa na Bwana wetu Yesu.
Wengi walishangaa, wengine hawaamini,
Wasema si yeye, kwamba wamefanana tu.
Wengine wahoji, awezaje mwenye dhambi,
Kufanya ishara na maajabu haya?
Wakashangaa na kupindisha maneno,
Eti Yesu mdhambi hawezi kuponya kipofu.
Kijana kajibu, mimi sijui zaidi,
Najua neno moja tu:
Nalikuwa kipofu, lakini sasa naona,
Nimeponywa na Yesu Mnazareti.
Simama imara, tetea imani yako,
Simama tangaza injili ya Yesu.
Simama imara, eneza upendo wa Yesu,
Ya kwamba ni Bwana naye anaokoa!
Watashangaa, mbona ni yule jambazi,
Aliyekuwa akiua watu wengi?
Watashangaa, mbona ni yule tasa,
Leo anyonyesha tena watoto mapacha?
Watashangaa, mbona ni yule mchawi,
Amekuwa akiloga watu wa Mungu?
Leo ahubiri injili yake Yesu,
Yesu kabadili historia yake,
Sio jambazi, sio mchawi, sio tasa,
Wote ni Bwana!
Simama imara, tetea imani yako,
Simama tangaza injili ya Yesu.
Simama imara, eneza upendo wa Yesu,
Ya kwamba ni Bwana naye anaokoa!
Njoo kwa Yesu, njoo na mizigo yako,
Haijalishi mizito kiasi gani.
Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu kama bendera,
Yesu azisafisha ziwe nyeupe.
Kwa Yesu yote yawezekana.
Haijalishi historia yako mbaya,
Yesu aita: "Njoo!"
Njoo abadili maisha yako,
Yesu aita: "Njoo!"
Njoo, njoo abadili maisha yako!