[male
vocals] (
Gentle
acoustic
oud
melodies
drifting
over
a
steady,
light
coastal
percussion)
Mpendwa
Dalia,
Salam!
Nakusalimu
kutoka
kilindini
mwa
moyo
wangu.
Salamu
ninakutumia,
zavuka
bahari
na
mawimbi,
Nina
shauku
kubwa
kukujulisha
jinsi
moyo
wangu
unavyohisi
kuuona
mkono
wako
wa
ukombozi.
Nina
shauku
ya
kuandika
na
kukushukuru
kwa
kunitupia
kamba
na
kunitoa
katika
shimo
refu
nilililozikwa
nikiwa
hai.
Nimekubali
kuwa
mateka
chini
yako,
huu
ni
ukweli
thabiti
kwangu.
Uwepo
wako
kwangu
umenifanya
niamini
kuwa
mfu
anaweza
kufufuliwa
na
kuishi
katika
dunia
nyingine.
Nimefufuka.
Nimefufukia
katika
ngome
yako,
nimeafiki
mapigo
ya
midundo
ya
ngoma
yako.
Kama
hili
litakuwa
kosa,
basi
wacha
iwe.
Nimekubali
kosa
na
nipo
tayari
kuadhibiwa
kwa
hili
nitendalo.
Nina
furaha
isiyoneneka
kukubali
kuwa
mtumwa
chini
yako,
katu
sitalijutia
kosa
hili.
Nitume
nikutumikie.
Nina
furaha
isiyoelezeka,
lazima
nitafurahia,
nitafurahia
uzuri
wa
uumbaji
wa
Mwenyezi
Mungu,
nitafurahia
zawadi
adhimu
ya
jina
lako
katika
maisha
yangu,
nitakufurahia
wewe
na
tumbo
lililokuzaa…..
wewe
ni
mshindi
na
shujaa
uliyeishinda
himaya
yangu.
Chambilecho
wahenga, “
kijakazi
msifadhila
haimfai
nyumba
ya
bwana
wake”………
Kwangu
hili
ni
bayana
lisilo
ajizi,
siwezi
kulipinga.
Dhamiri
yangu
inaupokea
na
kuuafiki
ukweli
huu
bila
walakini
yoyote.
Niko
mbele
yako,
najitolea
nafsi
na
hisia
zangu,
najitolea
maisha
yangu
kwako.
Wewe
ni
kurunzi
linalomulika
mapito
yangu
yenye
ukungu
mzito.
Ni
njia
iliyo
mororo
kuelekea
furaha
ya
maisha
yangu,
umetengua
vifungo
vya
uhuru
wa
nafsi
yangu.
Nitafurahia
hili
leo
na
kila
siku
nitafurahia……
nitafuarahia……..
Nitafurahia
kwa
sababu:
Mimi
ni
mja
niliyeonja
adha
ya
dhiki
Niliyechapwa
fimbo
ya
ghadhabu
na
mateso
Niliyechapwa
viboko
vya
macho
Mbele
sikuona!
Nilishikwa
na
mtesi,
jambazi
asiye
na
huruma
Aliniburuza
katika
makorongo
na
mawe
Akanitupa
katikati
ya
uwanda
na
wanyama
wakali.
Haikuwa
sekunde,
haikuwa
dakika,
haikuwa
saa
Haukuwa
mchana,
haukuwa
usiku
Hakutaka
kunihurumia.
Katika
shingo
yangu
alikunja
magoti
yake
Akanishinda
kwa
kutumia
mabavu
na
nguvu
zake
Hakujali
sauti
na
kilio
changu
Kwamba
pumzi
imeniishia
Siwezi
kupumua
tena!
Kisu
cha
moto
kilikwaruza
fundo
za
koromelo
langu
Nilivuja
damu
katika
mtima
wangu.
Nilikuwa
kama
mfu
ninayepumua
Nilikuwa
mfu
ninayemtazama
mtesi
wangu
Kama
mbuzi
wa
kafara,
sikuacha
kulia.
Alinizinga
mashariki
na
magharibi
Kusini
na
Kaskazini
Katikati
ya
anga
sikuona
mwanya
wa
kutokea
Nilifungwa
pingu
nzito
mikononi
mwangu
Hima
nililia
na
kuomba
usaidizi
Nani
aliyejali?...
lah!
Nilitanga
kama
mbuzi
anayetolewa
roho!
Nililia
kwa
machozi
jasho
na
damu
Hakuna
aliyejali
sauti
na
wangu
uchungu
Mtesi
na
ujahili
wake
alipamba
moto.
Alinizinga
kama
mnyama
afaaye
kwa
kitoweo
Aliziba
njia
zangu
zote
kushoto
na
kulia
Kwangu
ilikuwa
ni
kama
kifaranga
Aliyeachwa
na
mamaye
Nilifanywa
mkiwa.
Aliyatoa
makucha
yake
Yaliyokuwa
ndani
ya
maficho
asilia
Akaing’
ofowa
nyamangu
Nilikuwa
kituko
mbele
ya
dunia
Nilikuwa
aibu
isiyofichika
Nilijazwa
uchungu!
Nikajuta!
Ndoto
zangu
zote
zilizimika
Ni
zamani
za
ujinga
wangu
Kabla
macho
yangu
hayajaishika
sura
yako
Kabla
nafsi
yangu
haijaonja
utamu
wa
pendo
lako
Kabla
akili
yangu
haikuteua
jina
lako
katika
kamusi
la
dunia
Sikujua
kama
ningecheka
tena!
Uwepo
wako
kwangu
Umeifufua
pumzi
yangu
iliyozizima
Umeniwekea
nafsi
mpya
ndani
yangu
Umenipa
sababu
ya
kujiona
mtu
miongoni
mwa
watu
Umeifanya
nafsi
yangu
kuwa
rafiki
wa
amani
Mimi
si
takataka
tena
Mimi
si
kinyaa
tena
Mimi
si
kikaragosi
cha
wasiojua
thamani
ya
kupenda
Kwa
hili…….!
Nikijisahau
Nikashindwa
kukushukuru
Nitapigwa
kofi
la
anguko
takatifu
Nitapigwa
anguko
la
Firauni
Nitapigwa
upofu
na
kiza
kitanishinda
Nitawaudhi
mizimu
na
malaika
Kwa
kukosa
fadhila!.....
Nakushukuru!
Ndimi
nikupendae,
mpenzi
Jalia