Vijana nawakumbusheni, muda ndiyo nishani
Ukiona wewe spesho, waweza kuwa mbumbumbu kesho
Ukilala sana leo, jua malipo kesho
Mwana ujieleavyo ndivyo ukuavyo
Muda unaopoteza leo yaja yake matokeo
Wenzio wanaojituma, kesho yao ni spesho
Jifunze kujitegemea, acha kusubiri kukemewa
Ukidekedaka deka leo, utatepeta kesho
Muda ndiyo nishani, kama wabisha utaishia jalalani
Fanya kazi kwa bidi bila shuruti ya nje
Ndiyo nufaa maishani, kumiliki na kutunza
Lala sana ukitegemea cha wazazi, palilia umaskini wako
Unategemea wazazi wasiolala ili wewe ule na kulala
Wazazi watakuacha na dunia itakupokea
Umezoea vya bure sasa utalala bureee
Wewe ni buree usipojifunza leooo
Hakuna bure ndani ya Maisha ya leo
Jifunze kutoka kwa watangulizi walioona mengi
Iga kwa uzoefu, maana waona matokeo
Kila mahala wapo waliofanikiwa na historia yao ipo
Wapo wanaolipia gharama ya kupuuzia utotoni
Wapo walikufa kwa kushindwa kufanya kazi duniani
Wapo wanaoiba wakidhani kazi ni kukaba
Hakika kila mbegu unayopanda leo, baadae utavuna lake zao
Kijana pambana, fanya kwa bidi na maarifa
Ongeza bidii ya kidigitali ili ushinde thamani ya mentali
Fanya kimkakati, uongeze thamani, ubobee duniani
Jifunze kwao usidhulumu vyao, kwani karma nayo nayo ni kikwazo
Saidia wanaochipukia ili nao wawe makini pia
Mafanikio yako yajikite kuongeza mtaji na kukua
Tumia mtaji watu, ujipatie mtaji fedha na mtaji baraka ni matokeo